Mama Msamaria

26.10.2021 | Donne Europee, Donne Europee others

 

Alikuwa mama mmoja kwa moyo mzito. Alibeba mtungi wa maji, begani. Wakati huo jua kali sana, ilikuwa

saa sita mchana. Akaenda kuteka maji kisimani. Alikuwa mama mwenye sifa mbaya. Hakuweza kwenda kisimani wakati wa jioni. Hakutaka kukutana na watu wengine kijijini. Alikuwa hana marafiki. Wote walijua katika kijijini shida zake.

Siku ile alipokuwa bado mbali, akashangaa, akamwona bwana ameketi kisimani. Alikuwa kama amechoka sana. Alipokuwa karibu na kisima.. Akaona kwamba yule bwana ni Myahudi. Akawaza sana, kwa nini yule mtu yupo hapa. Wayahudi waliwachukia sana wasamaria. Hawakutaka kupitia Samaria, wakazunguka mbali sana.

Yule bwana alipomwona mama akasema : Nipe maji ninywe.” Yule mama Msamaria akashangaa tena zaidi: ” Imekuwaje wewe, mimi ni mwanamke Msamaria.”

Bwana akajibu:”Ungalijua karama ya Mungu naye ni nani akuambiaye, nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye naye ankalikupa maji yaliyo hai. ” Yoh 4:10

Mama akashangaa. Bwana akaendelea:” Ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele.” Mama akamwambia:”Bwana unipe maji hayo nisione kiu, wala nisije hapa kuteka maji.

Bwana akasema:” Nenda umwite mumeo, uje naye hapa.” Mama akajibu:” Sina mume.”

”Umesema kweli umekuwa na waume watano, uliye naye sasa siye mume wako. Umesema kweli.

 

Bwana Yesu na yule mama wakaendelea kuzungumza. Mama akasema:” Najua ya kuwa yuaja Masihi, aitwaye Kristo.”

Yule mama akauacha mtungi wake akaenda zake mjini, akaeleza mambo yote. Mama akaona kwamba yule bwana amejaa upendo na ufahamu na mwenye huruma. Mama alimkubali Yule Bwana Yesu Kristo moyoni mwake. Warumu 3:28 Lazima kubali dhambi zake, tena lazima amtegemee Bwana Yesu Kristo yaani amwamini.

 

Yesu Kristo anajua yote, hata mambo yote katika maishani mwetu. Hatuwezi kuficha hata kidogo.

Tuwe wazi mbele za Yesu Kristo. Yeye anataka kutusaidia. Yesu anakuambia leo: Usiogope, nitakupa maji yaliyohai. Nitasamehe dhambi zako zote. Nitakupa maisha mapya.” Uwe kama Mama Msamaria, aliyemkubali Yesu Kristo.

Yule mama akuacha mtungi wake, akaenda zake mjini. Labda wewe unabeba mtungi wako na ni mzito sana.

Acha mtungi wako kwa Yesu Kristo. Yeye anabeba mzigo wako.

Mungu akubariki

Armi Takala